Spark plugs work..
Spark plug kazi yake kuu ni kutoa cheche (spark) ndani ya silinda ili kuwasha mchanganyiko wa hewa na mafuta wakati unaofaa.
Kazi zake ni:
- Kuwasha mchanganyiko wa hewa na mafuta kwenye silinda.
- Kusaidia injini kuwaka na kufanya kazi vizuri bila kutetemeka.
- Kuboresha matumizi ya mafuta ikiwa spark plug iko katika hali nzuri.
- Kupunguza uchafuzi wa mazingira, kwa sababu mwako unakuwa kamili zaidi.
Dalili za spark plug mbovu ni pamoja na:
- Injini kuwaka kwa shida.
- Injini kutetemeka (misfire).
- Gari kukosa nguvu.
- Matumizi ya mafuta kuongezeka.
- Taa ya Check Engine kuwaka.
Maoni