CVT transmission fluid Change..
Kwa ujumla, CVT transmission fluid inashauriwa kubadilishwa kati ya kilomita 40,000–60,000, hasa kama gari linatumika kwenye mazingira magumu (foleni nyingi, joto kali, milima, au kubeba mizigo).
Kwa matumizi ya kawaida, baadhi ya watengenezaji huruhusu hadi 80,000–100,000 km, lakini mafundi wengi hupendekeza usisubiri kufika hapo kwa sababu kubadilisha mapema husaidia kuongeza maisha ya CVT.
Dalili zinazoonyesha fluid inaweza kuhitaji kubadilishwa ni pamoja na:
Gari kutetemeka wakati wa kuondoka.
Mabadiliko ya mwendo kuwa yasiyo laini.
Kelele kutoka kwenye transmission.
Kuchelewa kuitikia unapoweka D au R.
Fluid kuwa nyeusi au kunuka kama imeungua.
Muhimu: Tumia CVT fluid inayopendekezwa na mtengenezaji wa gari. Usitumie ATF ya kawaida kwenye CVT isipokuwa imeelekezwa na mtengenezaji.
By.Joseph Naftari Mujungu
Maoni